WAFANYABIASHARA WAFUNGA BARABARA ARUSHA

WAFANYABIASHARA wadogo wa matunda na mboga wanaoendesha shughuli zao eneo la Jacaranda, jana walifunga barabara ya Old Moshi kwa zaidi ya saa mbili wakipinga kitendo cha Halmashauri ya Jiji kuvunja vibanda vyao saa 10:00 alifajiri. 

Walifunga barabara hiyo kwa kutumia mabaki ya matunda, mboga, mbao na chuma walizokuwa wakitumia kuhifadhi vitu hivyo hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara huku ikonekana misururu mirefu ya magari na pikipiki iliyokuwa ikitokea katikati ya Jiji na ile iliyotokea maeneo ya Kijenge, Moshono na Njiro.

Wafanyabiashara hao walifunga barabara hiyo kwa nyakati mbili tofauti ambapo saa moja asubuhi, walifunga kwa mara ya kwanza ambapo waliifungua saa 2 asubuhi baada ya kuombwa na polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa wakipita eneo hilo.

Hata hivyo, ilipofika saa 3:30 asubuhi, waliamua kuifunga mpaka saa 5:00 alipofika mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), Meya Gaudence Lyimo (CCM) na baadhi ya madiwani wa jiji.

Wazungumza eneo la tukio, wafanyabiashara hao walikiri kupokea barua kutoka kwa mkurugenzi wa jiji akiwataka mpaka Agosti 22, mwaka huu, wawe wameondoka na kuhamia eneo la Relini kata ya Themi na soko la Kijenge.

“Sisi tulikuwa tunasubiri waje wakatuonyeshe hayo maeneo waliyotuambia twende, kwa sababu hatuwezi kwenda kugawana kienyeji. Tukaona hawaji, ijumaa tulienda kwenye ofisi ya mkurugenzi, akatuambia anakwenda kwenye kikao.

“Tulikaaa pale mpaka saa 8:00 mchana, tukafanikiwa kuonana na Meya Lyimo akatuambiua tusiondoke, atakuja na diwani wetu leo saa 2 asubuhi ili wakatukabidhi hayo maeneo lakini tumeshangaa saa 9 alfajiri napigiwa simu mlinzi kakamatwa vibanda vimevunjwa na mali zimechukuliwa,” alisema mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Richard Isaya.

Baadhi ya wafanyabiashara hao walionekana wakilia huku wengine wakipoteza fahamu ambapo mmoja wao, Florah Zakaria, alisema kuwa yeye ni mjane na alianza kufanya biashara kwenye eneo hilo mwaka 1985.

Lema na Meya
Lema alisema kuwa uharibifu uliofanywa na halmashauri haukubaliki na kwamba ni lazima wafanyabiashara hao walipwe fidia huku kwa madai uvunjaji huo umekiuka sheria.

“Kuharibu chakula hivi hii ni laana na haikubaliki, tumewakimbiza wamachinga mjini kwa nguvu sasa hata hatuwezi kuelewa haya matukio ya kihalifu ya kutumia risasi kwa nini yameongezeka.
Naye meya Lyimo, alikiri kukutana na wafanyabiashara hao juzi na kupanga kukutana nao jana asubuhi huku akisisitiza kuwa tayari alikuwa ameshaongea na mkurugenzi wa jiji kuwa wasiondolewe wote kwani kuna waliokuwa hapo muda mrefu.

Alisema kuwa walishauriana kuboresha mazingira ya biashara hiyo ikiwemo kutengeneza matoroli yatakayokuwa na friji yatakayowezesha matunda hayo kudumu muda mrefu bila kuharibika na watapelekwa kwa muda maeneo ya Relini, Brewaries na Kijenge ili eneo hilo lijengwe.

CREDITS:TANZANIA DAIMA
WAFANYABIASHARA WAFUNGA BARABARA ARUSHA WAFANYABIASHARA WAFUNGA BARABARA ARUSHA Reviewed by habari motto on 10:40 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.