Mwili wa kijana huyo ukiwa katika gari la polisi kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
KIJANA anayesadikiwa
kuwa kibaka na ambaye hajafahamika jina lake, leo asubuhi amechomwa
moto hadi kufa akidaiwa kuiba baiskeli maeneo ya Nane Nane mjini
Morogoro, jirani na shule ya Sekondari ya Alfa James ambayo ni maarufu
kama Shule ya Father Pekupeku.
”Majira ya saa moja asubuhi tumeona
vijana wanne wakimfukuza mwenzao, walipofika hapa kwenye mabweni ya
shule ya Alfa, wakamkamta akiwa na baiskeli na kumshushia kichapo kikali
na baadaye wakamchoma moto wakidai alikuwa ameiba baiskeli yao maeneo
ya Tubuyu, ” alisema shuhuda mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la
Mama Happy.
Gari la polisi likiondoka na mwili wa kijana huyo.
Wanafunzi wa Sekondari ya Alfa James wakishuhudia mahali alipochomewa mtuhumiwa.
Raia wengine waliofika eneo la tukio.
Mtandao huu wa paparazi ulishuhudia
kijana huyo akiendelea kuteketea kwa moto akituhumiwa kuiba baiskeli
kuukuu yenye thamani ya shilingi 60,000. Polisi walifika na kuuchukua
mwili huo na kuupeleka Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Wanafunzi wa Sekondari ya Alfa James wakishuhudia mahali alipochomewa mtuhumiwa.
Raia wengine waliofika eneo la tukio.
ACHOMWA MOTO AKIDAIWA KUIBA BAISKELI
Reviewed by habari motto
on
6:07 PM
Rating: