NYUMBA YA MFANYABIASHARA ZANZIBAR YAUNGUA MOTO

Nyumba hiyo ikiwa imeteketea kabisa. Nyuma inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu mjini Zanzibar, Noushad Mohammed Suleiman, iliyopo mtaa wa Kwa Kisasi barabara ya Bububu, imeteketea kwa moto. Nyumba hiyo yenye vyumba vitatu na msikiti, iliungua jana jioni kutokana na hitilafu ya umeme.
Mfanyabiashara Noushad Mohamed Suleiman akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuungua nyumba yake. Moto huo umeathiri vibaya nyumba hiyo, pamoja na samani zote zilizomo ndani. Akizungumza na waandishi wa habari hizi, mmiliki wa nyumba hiyo alisema, chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, ambao ulianzia katika chumba cha kushonea na baadae kuenea sehemu nyengine. Vitu vingine vilivyoungua ni nyaraka muhimu, hati za kusafiria za watoto wake, televisheni seti sita, friji mbili, kuka, viyoyozi sita na samani za vyumba vyote na kumbi. Alisema thamani ya vitu vilivyoungua bado haijajulikana.
Gari za vikosi vya zimamoto zikiwa katika eneo la tukio. Hata hivyo, alikishukuru Kikosi cha Zima Moto na Uokozi (KZU) pamojana wananchi kwa ushirikiano wao uliofanikisha kuudhibiti moto huo. Noushad ambae ni mfanyabiashara mkubwa, alisema ingawa nyumba hiyo haijakatiwa bima, hana wasi wasi na kwamba katika kipindi kifupi atajenga tena nyumba hiyo. Naye Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa mjini, Ame Ali Suleiman, alisema walipata taarifa ya moto huo kupitia simu ya mkononi majira ya saa 10:07 za jioni na walifanikiwa eneo la tukio saa 10:17.
Vikosi vya zimamoto vya ZKU vikijitahidi kupambana na moto huo. Alisema waliudhibiti moto huo uliokuwa ukiwana kwa kasi kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma. Akizungumzia changamoto walizokumbana nazo wakati wa uzimaji moto huo, alisema hawakuwa na maji ya kutosha hali iliyowalazimu kurudi tena mjini kufuata maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa mjini magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, alisema hakuna mtu alieathirika na moto huo wala hakukua na uhalifu wa aina yoyote ulioripotiwa. Aliwataka wanachi kuwa na tahadhari wanapotumia vitu vya umeme, pamoja na kuhakikisha wanazima vitu vyote wanapomaliza kutumia
NYUMBA YA MFANYABIASHARA ZANZIBAR YAUNGUA MOTO NYUMBA YA MFANYABIASHARA  ZANZIBAR YAUNGUA MOTO Reviewed by habari motto on 7:23 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.