MAKABURI 2514 YA ARUSHA KUAMISHWA


MAKABURI  2, 514 yaliyopo eneo la Stendi Ndogo Jijini Arusha yanatarajia kuamishwa na miili ya marehemu hao kuzikwa tena kwenye makaburi yaliyopo eneo la Njiro  lengo ni kupisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo stendi ya kisasa ya kushusha na kupakia abiria.

Hayo yalisemwa leo Jijini hapa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,Juma Idd wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mipango mbalimbali inayotekelezwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha Jiji linakuwa na mpangilio wa kisasa.

Alisema makaburi hayo yanatarajia kuamishwa muda wowote kuanzia sasa kwani taratibu zote za kidini zimeshafuatwa ikiwemo maongezi baina ya viongozi wa Jiji la Arusha akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Jijini hapa.
MAKABURI 2514 YA ARUSHA KUAMISHWA MAKABURI 2514 YA ARUSHA KUAMISHWA Reviewed by habari motto on 4:30 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.