Mchina akichezea kichapo kwa kumshika mke wa mtu maziwa mjini Iringa
RAIA mmoja wa Kichina ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayesadikika kuwa ni mmoja kati ya mafundi katika ghorofa moja mjini Iringa amejikuta akichezea kichapo kutoka kwa njemba mmoja ambae alikuwa ameongozana na mke wake baada ya mchina huyo kumshika maziwa mwanamke huyo akimtaka mapenzi mbele ya mumewe .
Tukio hilo lililofananishwa na udhalilishaji kwa wanawake lilitokea jana majira ya saa 2 usiku katika eneo la stendi ya daladala za Mkwawa kata ya Miyomboni mjini Iringa.
Kutokana na kitendo hicho cha aibu alichokifanya mchina huyo mume wa mwanamke huyo alikosa uvumilivu na bila kujali kuwa wachina ni wataalam wa kareti alimvaa mchina huyo na kumpiga mtama uliopelekea kuanguka chini na kuwafanya vijana wapiga debe eneo hilo kuanza kumshambulia kwa kichapo bora mradi wamepigana na mchina .
Vijana wakimpa kichapo mchina huyo |
Hapa akionyesha eneo lake la kazi
DONATE CAR TO CHARITY CALIFORNIA
Kichapo kikali alichokipata mchina huyo ambae muda wote alikuwa akilalamika kwa kilio cha kichina ilimfanya mmoja kati ya askari anayeendesha biashara zake eneo hilo anayetambulika kwa jina moja la Rashid kufika kunusuru ugomvi huyo na baada ya kutamkiwa Polisi mchina huyo alipiga magoti na kuonyesha ishara za kutubu kosa na askari huyo alisikika akisema umefanya kosa huwezi mshika mwanamke maziwa hadharani na kuachiwa .
SHUHUDIA HAPA; MCHINA ACHEZEA KICHAPO KWA KULAZIMISHA PENZI KWA MKE WA MTU
Reviewed by habari motto
on
10:20 AM
Rating: