STEVE NYERERE AKUBWA NA AIBU YA AINA YAKE

NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa ‘kihasarahasara’.Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0. Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani (zinazotumiwa na Yanga).

Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara hadharani.
STEVE NYERERE AKUBWA NA AIBU YA AINA YAKE STEVE NYERERE AKUBWA NA AIBU YA AINA YAKE Reviewed by habari motto on 2:30 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.