SUPER STAR MAINDA AFUNGUKA KUHUSU MUME MTARAJIWA

STAA wa filamu Bongo ambaye amejikita kumtumikia Bwana kwenye wokovu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kamwe hawezi kuainisha sifa za mwanaume anayehitaji aolewe naye kama ilivyo kwa mastaa wengine kwa kuwa jukumu hilo ni la Mungu. 

Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Mainda alisema japo umri wake unaruhusu kuolewa hawezi kuweka wazi sifa za mwanaume anayehitaji awe wake kwa kuwa huenda sifa anazozihitaji Mungu hajampangia kuolewa na mtu wa aina hiyo.“Kwenye maono naona kabisa mume wangu yupo karibu ambaye Mungu ameniandikia, sasa siwezi kusema nahitaji mwanaume mwenye sifa zipi sababu nikisema nahitaji awe hivi kumbe Mungu hajanipangia huyo,” alisema Mainda.

SUPER STAR MAINDA AFUNGUKA KUHUSU MUME MTARAJIWA SUPER STAR MAINDA AFUNGUKA KUHUSU MUME MTARAJIWA Reviewed by habari motto on 8:28 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.