Huu Ndiyo Utajiri Wa Msanii Masanja Mkandamizaji

 Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake. UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi. HABARI MEZANI Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo. “Masanja sio yule tena.


 Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu. Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini
Huu Ndiyo Utajiri Wa Msanii Masanja Mkandamizaji Huu Ndiyo Utajiri Wa Msanii Masanja Mkandamizaji Reviewed by habari motto on 8:12 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.