Msanii Geez Mabovu Afariki Dunia

http://photos-c.ak.instagram.com/hphotos-ak-xap1/10810035_344277472418210_1007440266_n.jpg

Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2

Geez 3
Hii ni picha ya July 2013 ambayo ni mara ya mwisho Geez Mabovu ameonekana kwenyebekamtanzania.com akiwa na Baba yake Dully Sykes maeneo ya Kinondoni Dar es salaam nje ya Bar ya msanii Dudubaya aliyokua ameifungua wakati huo.
Dennis ambae alikua mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha pia kuhusu kifo cha Geez Mabovu na kusema rapper huyu aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.
Kwa mujibu wa Denis, Geez atazikwa kesho jioni November 13 2014. #RIP
Msanii Geez Mabovu Afariki Dunia Msanii Geez Mabovu Afariki Dunia Reviewed by habari motto on 2:36 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.