Basi la Wibonela linalofanya safari zake kati ya Kahama - Dar limepinduka na kupelekea zaidi ya watano kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhi vibaya,ajali hiyo imetokea mapema leo katika eneo la Fantom nje kidogo ya mji wa Kahama. Chanzo kinaelezwa ni mwendo kasi uliopelekea kumshinda dereva wa basi hilo wakati akikata kona ya kuingia barabara kuu hali iliyopelekea basi kupinduka. Taarifa kamili tunaendelea kuifatilia na tutaendelea kujuzana hapa hapa.
Sehemu ya Mashuhuda wa ajali hiyo wakiendele kuchukua taswira mbali mbali wakati jitihada za kulinyanyua gari hilo zikiendelea.
| Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la ajali leo asubuhi |
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt Joseph Ngowi amesema watu waliopoteza maisha katika ajali ya basi leo asubuhi mjini Kahama ni wanne ambao ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa Kigoma, Salum (amefahamika kwa jina moja) mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja huku majeruhi wakiwa 41.
Tukio hilo limetokea leo saa 12 asubuhi katika eneo la Phantom kilomita chache kutoka Stand ya Mabasi mjini Kahama baada ya basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.
Chanzo cha habari cha Malunde1 blog kimesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kuendesha mwendokasi wakati akitoka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama na alipofika kwenye kona ya kutoka mjini Kahama kuelekea Isaka basi lilimshinda huku yeye akiruka kutoka kwenye gari na kuangukia katika mtaro na basi kupinduka.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dkt Joseph Ngowi amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Maulid Shaban (44) mkazi wa Ushirombo, Athuman Issa (21) mkazi wa Kahama, Jordan Mbeya (28) mkazi wa Kasulu, Brandina Patrick (24) mkazi wa Kasulu, Oscar Lameck (19) Mkazi wa Kigoma, Stamili Shaban (38) mkazi wa Dodoma, Neema Dastan (18) Mkazi wa Kahama na Monica Gadson (35) mkazi wa Kahama.
Majeruhi wengine ni Nickson Andati ambaye ni Mchungaji mkazi wa nchi ya Rwanda (34) Lucas Mlezi (48), Joyce Fred (28) Asnati Remtula (27) , Eveline Hamis (6), Happy Hamis (30), Japhet Masha (29), Jackson Elisanto (26), Buligelila Ramadhani (40) na Rita Bryson (25) wote wakazi wa Kahama.
Pia kuna Irene Wilson (17) mkazi wa Kasulu, John Lembo(45) Mkazi wa Bariadi, Hamis Shaban (31) mkazi wa Kahama, Emmanuel Lambambo (32) mkazi wa Kigoma, Kashindye Masanja (28), Frenk Kishimba (21) Peter Bahati (22) wote wakazi wa Kahama, Iseme Ilila (36) mkazi wa Katoro Geita, Ebrania Saga (30) mkazi wa Kigoma, na Anika Amdani (35) Mkazi wa Kahama.
Wengine ni Shaban Omary (16) ambaye ni mkazi wa Dodoma,Grolia Moses (18) mkazi wa Kahama, Agnes Broto (35) Mkazi wa Ngara, Kulwa Said (40) mkazi wa Kahama, Peter David (42) mkazi wa Kahama,Tunga Lazaro (22) mkazi wa Mariadi, na Happy David (32) huku majeruhi wengine wakishindwakutambulika kutokana na kuwa mahututi.
Miili ya marehemu ipo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
NA Malunde1 blog
Taarifa Kuhusu Ajali Ya Basi La Wibonela, Majina Ya Majeruhi Na Marehemu
Reviewed by habari motto
on
5:17 PM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
5:17 PM
Rating:



