Baada Ya Kipigo, Mourinho Asema Haya

Bosi wa klabu ya Chelsea, mreno, Jose Mourinho ameelza kipigo cha timu yake toka kwa Newcastle kama bahati kufuatia kupoteza kwa mara ya kwanaza toka msimu huu uanze. Hata hivyo bosi huyo (Mourinho) amewanyooshea vidole vijana waokota mipira wa Newcastle United (ball boys) huku akisema timu bora imepoteza.
ch
Katika mchzo huo Chelsea ilionekana kama ingeibua na ushindi baada ya kuanza vyema uwanjani hapo lakini ikajikuta ikipoteza kwa magoli ya msenegali Papiss Cisse kunako dakika za 57 na 78.
Hata hivyo, kuingia kwa bao hizo hakukuwafanya wakate tamaa kwani klabu hiyo iliendelea kupambana kurudisha goli hizo hasa baada ya mchezaji wa newcastle Steven Taylor kuoneshwa kadi ya pili ya
manjano kunako dakika ya 81 na kutolewa nje, ambapo mkongwe Didier Drogba aliifungia timu hiyo goli la kichwa kufuatia mpira wa adhabu toka kwa Cesc Fabregas lakini wenyeji walifanikiwa kulinda lango lao pamoja na kuwa na kipa chipukizi Jak Alnwick kunako kipindi cha pili
“hatukuwa na bahati” alinukuliwa meneja huyo katika nukuu za klabu hiyo kwenye mtandao wa Twitter. Timu bora imefungwa, timu iliyojitahidi kusaka ushindi, ndo mpira”. Akaongeza “ni matokeo ambayo inabidi ukubaliane nayo, hatukuwa na bahati, tumefungwa pale tu walipofanikiwa kuvika msitari wa katikati”
Kwa matokeo hayo klabu ya Chelsea imepokea kipigo cha kwanza msimu huu katika uwanja wa St James’ Park huku kocha huyo mwenye maneno mengi akisema waokota mipira pia walisababisha ugumu kwa kikosi chake ingawa kirekodi hajawahi kushinda nyumbani kwa newcastle katika mechi za ligi.
“tulitaka kucheza zaidi na zaidi, ila kuna wakati ilikua ngumu kwa kile ninachoweza kusema uwepo wa mambo ambayo huyatarajii katika soka endelevu, mipira ilipopotea, kuna wakati haikuja, kuna wakati ilikuja na kuja, vijana waokotaji wakatoweka, hali kama hizi bado zipo katika mchezo huu hivyo silaumu” aliongeza bosi huyo
Kwa upande mwingine kocha huyo hakutaka kuwalaumu nyota wake akisema “wachezaji wangu walijitahidi kila walichoweza, siwalaumu, nawapongeza Newcastle. Ningesikitika kama kufungwa kungetokana na uchezeshaji wa refarii au kiwango kibovu cha timu yangu, lakini ni vile tu hatukuwa na bahati, iko siku tuatakua na bahati”
Baada Ya Kipigo, Mourinho Asema Haya Baada Ya Kipigo, Mourinho Asema Haya Reviewed by habari motto on 1:53 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.