Baada Ya Kuzushiwa Kufariki, Kocha Kibadeni Afunguka

Kocha maarufu nchini, Abdallah ‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.

Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara.

“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.

“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.

“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.

“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.SALEHE JEMBE BLOG
Baada Ya Kuzushiwa Kufariki, Kocha Kibadeni Afunguka Baada Ya Kuzushiwa Kufariki, Kocha Kibadeni Afunguka Reviewed by habari motto on 10:21 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.