Hatimaye Rihanna Abeba Mimba


rihannacroppedTOVUTI ya MediaTakeOut imesema mwanamuziki Rihanna ni mjamzito asilimia 100 na ina vithibitisho kuhusu taarifa hiyo na kama siyo kweli watatoa Dola za Kimarekani 10,000.
Katika ripoti iliyotolewa na tovuti hiyo, inadaiwa kuwa Rihanna ni mjamzito na walipata taarifa hizo jana huku wakieleza kuwa si tetesi taarifa hizo ni za uhakika asilimia 100.
Mtandao huo uliongea na watu wawili tofauti waliokaribu na staa huyo waliouambia kuwa Rihanna kwa sasa ameelekeza nguvu katika wimbo wake mpya uliopo kwenye albamu yake ambapo ataelekezea
kuhusu ujauzito huo.
Rihanna was dressed in her sweats, sweatshirt, tennis shoes, hat and sunglasses as she went to the doctor in Beverly Hills
Mmoja wa watu hao alisema, “Katika wimbo huo Rihanna anaongelea mtoto anayeendelea kukua tumboni mwake”
Mbali na hilo, inasemekana staa huyo kwa sasa havuti bangi katika studio anazotumia kurekodia wimbo huo jambo ambalo ni ajabu kwa mrembo huyo ambaye anafahamika kwa kupuliza moshi kama dohari.Kusoma zaidi bofya
Inadaiwa pia mrembo huyo kwa sasa ana furaha kubwa kwa kupata ujauzito huo ambao aliugundua hivi karibuni.
Wadau wengi bado wana sintofahamu juu ya nani baba wa mtoto huyo huku wengine wakihisi kuwa huenda muhusika ni Drake.
Mtandao huo umezidi kunyetisha kuwa kuhusu mhusika wa mimba hiyo bado hauna uhakika ni nani ila wao wana uhakika 100% kuwa mnyange huyo ni mjamzito na iwapo kuna mtu anabisha dola 10,000
ziko mezani kwa ajili yake
Hatimaye Rihanna Abeba Mimba Hatimaye Rihanna Abeba Mimba Reviewed by habari motto on 7:50 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.