Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa jeshi la Polisi na wasamaria wema wanaendelea kuokoa majeruhi na maiti wa ajali ya gari iliyotokea muda wa masaa mawili yaliyopita kwa kuuhusisha basi la Unique namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.
Akizungumza nasi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa alibainisha kuwa, hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha huku 51, wakijeruhiwa vibaya na kuendelea kukimbizwa hospitali.
“Hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha. Na tunaendelea kuokoa wengine ambao 51 ni majeruhi. hivyo bado tupo hapa kwa sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa” RTO Chacha.
Hadi sasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.





Watu 10 wafariki dunia na 51 wajeruhiwa, ajali ya basi Shinyanga
Reviewed by habari motto
on
6:45 PM
Rating: