Waziri akizindua Transfoma na nguzo mbili za umeme; Mbunge Atoa Ufafanuzi

Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi ameibuka na kutolea ufafanuzi picha inayosambaa mitandaoni ikioonesha waziri wa nishati Dr.Kalemani akiwa na baadhi ya viongozi akiwemo mbunge huyo wa mafinga wakiwa wamesimama kwenye Transfoma ya umeme ikionesha kuna uzinduzi unafanyika.

Mh chumi ameeleza kwamba zoezi hilo lilikuwa la kuzindua mradi wa umeme vijiji(REA) awamu ya tatu  katika eneo la Lumwago, Mafinga.

"Tukio hili tulikuwa tunazindua umeme wa REA awamu ya tatu katika eneo la Lumwago, Mafinga. Pichani ni mimi Mbunge Cosato Chumi, Waziri wa Nishati Mhe Dr Kalemani, DC wa Mufindi Mhe J.D. William, kwa nyuma Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mhe Daud Yasin na viongozi mbali mbali".Ameeleza Chumi kupitia ukurasa wake wa Instagram

Picha hiyo iliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii huku watu wengi wakifikiria kwamba waziri alikuwa anazindua Transfoma na kushanga iweje waziri azindue Transfoma wakti ni kitu cha kawaida?.kumbe ukweli ni kwamba waziri alikuwa anazindua mradi mkubwa wa umeme vijijini.
Waziri akizindua Transfoma na nguzo mbili za umeme; Mbunge Atoa Ufafanuzi Waziri akizindua Transfoma na nguzo mbili za umeme; Mbunge Atoa Ufafanuzi Reviewed by habari motto on 6:12 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.