RISASI 40 ZAKAMATWA GUEST HOUSE


Kiasi cha risasi 40 za bastola zimekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya baada ya kufanya upekuzi moja ya vyumba katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Sogea Tours Hotel & Guest House iliyopo katika mtaa wa Sogea, Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jeshi la polisi mkoani hapa upekuzi huo ulifanyika jana saa 11 jioni katika mtaa wa Sogea, kata na tarafa ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoani Mbeya. Risasi zilizokutwa zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko wa plastiki maarufu kama Rambo na kuwekwa kwenye kasha lake na kisha kufichwa chini kwenye begi lililokutwa chumbani humo.
Pia Fichuo Tz imebaini kuwa upekuzi huo ulifanyika baada ya kupatikana taarifa toka kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni kuwa kunachumba kimojawapo ambacho tangu kikodiwe hakijafunguliwa na mtu aliyekikodi hajaonekana hivyo kusababisha hofu kubwa kwa wenyeji wa mahali hapo.
Akiithibitishia Fichuo Tz juu ya tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi ametoa wito kwa wananchi na wamiliki wa wa nyumba za kulala wageni na Bar kuwa makini na wateja wao au wageni wao na pindi wanapoona viashiria ambavyovisivyokuwa vya kawaida kutoa taarifa mara moja kwa jeshi la polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
RISASI 40 ZAKAMATWA GUEST HOUSE RISASI 40 ZAKAMATWA GUEST HOUSE Reviewed by habari motto on 7:43 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.